Chapati for dinnerπ½: , mlo wa jioni inapendeza ukiwa unabadilisha vyakula kila siku, isiwe usiku kila siku ni wali tu, badilisha vyakula viazi, chapati, tambi, ndizi nk.
Recipe Yangu ya chapati ni simple na ya uhakika, mtag pia rafiki yako anaye penda chapati;

Chapati recipe
π΄
Mahitaji
ππΏ
β ngano 1/2 kg
β mafuta 1/4 L
-chumvi kijiko kidogo 1
β maji 400 m/l
ππΏ
Jinsi ya kutengeneza Weka maji kwenye kibakuli (400 M/l) yawe ya uvuguvugu kisha tia chumvi na koroga vizuri ichanganyike.
ππΏ
Tia unga wa ngano katika bakuli kubwa ya kukandia, kisha tia mafuta kama vijiko vinne vikubwa katika unga. Kisha tia maji katika unga na anza kuukanda, kanda mpaka uone umechanganyika vizuri utengeneze donge moja kubwa. Ukimaliza anza kutengeneza vidonge vidogo vya duara, kama kwenye picha kisha unavipanga kwenye kibao. (angalia picha zinazo fata) ππΏ
Kisha unachukua moja moja unasukuma, unaweka frying pan yako jikoni ukipata moto unaweka chapati, unaigeuza pande zote mbili ipate moto kisha unaweka mafuta unakaanga upande wa juu ukiwa tayari unageuza upande mwingine unaweka mafuta unaikaanga ukiwa tayari unatoa, unafanya hivyo mpaka zote zinaisha.ππΏ
Chapati zako unaweza kula na chai, juisi au mchuzi wa nyama, maharage, mboga za majani au chochote utakachopenda.
.
.
.
.
#chapati #chapatirecipe
homecookingfood #simplerecipe #quickandeasyfood #africanfoods #africanfoodyummy #sweethomeπ‘ #africancooking # #foodfamily
.
. #tanzanianfood #foodbloggerlife #swahilifood #mapishi #jikoni #malkiawajiko #jifunzemapishi #jiko #tanzanianblogger #chakula #mapishiyakiswahili