CHIPSI MAYAI

Chipsi mayai aka TZ pizza🍳🍟, inawezekana mi ni mmoja wa watu wanao jua kupika chipsi mayai ikatoka vizuri kabisa;
– imekauka Bila rojorojo ndani
– Imekauka vizuri bila kuungua – Yai na chipsi vimeshikana vizuri
– Iko kavu haina mafuta mafuta mengi
😃😃 Jamani sifa jipe mwenyewe.
.


Kitu nacho mshukuru Mungu wanangu wanapenda na wanakula vyakula karibu vyote vya kitanzania. Chipsi mayai na kachumbari ya nyanya, kitunguu na ndimu hapo huwaambii kitu. Wako likizo hii nimewapikia mchana.
🍳
– Ok chipsi mayai ukitaka itoke vizuri, hakikisha chipsi zimeiva vizuri zikakauka, pia tumia mayai ya Kuku wa kienyeji au walau kidogo ya Kuku chotara. – Pima chipsi sahani moja weka frying pan jikoni Tia na mafuta vijiko 2 vikubwa, weka mayai 3 au 4, kwenye bakuli Tia chumvi kidogo yapiga pige na uma (sio kijiko) hadi uone yametoa makovu.
🍳
– washa jiko na weka frying pan jikoni, Hakikisha mafuta yamepata moto wa kutosha (yasiwe baridi yasiwe moto sana) weka chipsi kisha tia mayai, acha yaive km dk 1 na kisha geuza upande wa pili nako yape dakika 1. 🍟
Ukitaka kuwa na uhakika yameiva vizuri na kukauka hadi ndani, chukua uma jaribu kubonyeza juu ya chipsi Kwa nguvu ukiona rojorojo zinatoka basi hazija kauka vizuri acha kidogo ziive. Kisha test tena Kama the hamna rojorojo zinatoka jua zimeiva fresh. #karibuni

Published by eunicemahundi

Hi🙋🏾, Naitwa Eunice Mahundi, ni #foodblogger na napenda sana mapishi, wengi mna nifahamu kama Mjasiriamali Ila food blogging ni kitu kingine nacho kipenda sana. 🍲🍝🍹🍷🍚🍽 Mapishi Yangu huwa ni simple, Ila yanavutia na mengi ni swahili cuisine, pia huwa napost dondoo za jikoni kama; -Usafi -vyombo -ratiba ya chakula/mapishi -nk Karibu sana na ione malkia wa jiko blog kama nyumbani kwako, ujifunze mengi. Ukiwa na maswali, maoni au chochote kile wasaliana nami: 📧 eunicemahundi@yahoo.com Whatsapp : 0752 741 831or 0657 234 897

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started